Skip to content

Penzi wangu ucjali.

Maisha hapa chuoni, ni magumu mno sana Nafunga yangu machoni, ili kesho kuiona Sembe sukuma mezani, kutia tukizi sana Penzi wangu usijali nilikwacha nijikimu Nguo moja nimekita, sio eti ninapenda Hata nywele sijikata, juu juu zinapanda Nyayo kwako nimekata, taniua nishakonda Penzi wangu usijali, nilikwacha nijikimu Kazi yake muhazili, sitaweka hata chapa Kwa rehema za Jalali, hitatupwa kwebye pipa Kwa hakika sina hali, ni maisha nanichapa Penzi wangu usijali, nilikwacha nijikimu Za kukwenda kwenye mesi, hata kumi mimi sina Mkopaji kwenda mesi, limekuwa langu jina Ninajuta hiyo kasi, likwendavyo hilo… Read more Penzi wangu ucjali.

Yanga bingwa pinduzi.

***YANGA BINGWA MAPINDUZI*** ** * Paka havuki bahari, kwenda kuifunga Yanga / Katu hii siyo siri, kule Zenji wamelonga / Icheki yao dosari, ni baada ya kipyenga / Tumetwaa Mapinduzi, kwa kumfunga mtani //// * Imedhihiri #sadfa, kisiwa cha Zanzibari / Yanga kuipata sifa, ndani hii januari / Simba kapata kifafa, kalambwa kombe shuburi / Tumetwaa Mapinduzi, kwa kumfunga mtani //// * Viza kwenda kisiwani, Paka koko wamekosa / Wakashindwa ushindani, goli tukenda wanasa / Wananchi burudani, Simba tumempapasa / Tumetwaa Mapinduzi, kwa kumfunga mtani //// * Ni kombe la… Read more Yanga bingwa pinduzi.

Nampenda.

NAMPENDA😍😍😍 Nimezama mapenzini Na sitamani kutoka Nimempenda Fulani Na yeye ameridhika Hata mi mnipe nini Mimi kwake nimefika Nampenda kwelikweli Kumuacha abadani Kumuacha abadani Nathubutu kutamka Nyonga mkalia ini Huyu wangu muhibaka Amenikaa moyoni Katu hawezi kutoka Nampenda kwelikweli Kumuacha abadani Amenijaa kichwani Siachi kumkumbuka Hata nikiwa ndotoni Sautiye yasikika Namuomba RAHMANI Marengo kutimizika Nampenda kwelikweli Kumuacha abadani Nampa vitu laini Meno yasije kun’goka Biriani ya maini Ale pindi akitaka Nae kaniganda yani Hawezi kuchoropoka Nampenda kwelikweli Kumuacha abadani Anipenda si utani hatamani kuchepuka Mimi kwake ndie shani Nanga’ra nanawirika… Read more Nampenda.

Hana Taraka.

HANA TARAKA. Na tena mkitengana, hawara hana taraka, Wala hatongozwi tena, hawara ukimtaka, Tena mnapokutana, ya nyuma kuyakumbuka, Hana taraka hawara, ukweli nimebaini.. Nilikuwa ninabisha, kukataa jambo hili, Yanayo mengi maisha, mengine sio ya kweli, Hili nimethibitisha, kwa macho yangu mawili, Hana taraka hawara, ni kweli sio utani. Usije kudanganyika, Aseme wameachana, Mambo yatavurugika, siku watapokutana, Yalio sahaulika, yote watakumbushana, Hana taraka hawara, Chunguza utabaini.. Wasema umempata, na umfute machozi, Alomliza hufwata, tena bila ya ajizi, Akitakacho hupata, na kupeana mapenzi, Hana taraka hawara, hilo weka akilini.. (Malenga ni Ibn… Read more Hana Taraka.

Jitokeze nikuone.

JITOKEZE NIKUONE Yuko wapi nauliza, mwenye mapenzi ya dhati? Kipusa wa kupendeza, mtego kwa ‘tanashati? Asiyependa kuliza, na akipenda hasiti? Kipusa pale ulipo, jitokeze n’kuone. Aliye na umbo nzuri, aibuaye hisia? Mtamu kama sukari, ‘kimbusu najifia? Nihisi mie ushwari, na akinikisi pia? Kipusa pale ulipo, jitokeze n’kuone. Fundi wa kusasambua, tena bila kusumbua? Na kiuno kunengua, tena bila kutegua? Katu sitomzingua, ‘tampenda atambue, Kipusa pale ulipo, jitokeze n’kuone. (MTUNZI:Kongowea)

Mapenzi yanaumiza.

MAPENZI YANAUMIZA Bora uchomwe na mwiba Ukitoa utapona Sio utoswe na huba Kwa yule mlopendana Ukamwita mahabuba Leo haunae mbona Mapenzi yanaumiza Maumivu yasokwisha Chakula hautoshiba Hamu ya kula hauna Utachukia mahaba Hutaki kupenda tena Moyo wauma si haba Tena Unauma Sana Mapenzi yanaumiza Maumivu yasokwisha Machozi yanakukaba Kutoka yashindikana Wajuta majuto Saba Kwanini ulimuona Umeipata dhoruba Mapenzi kweli hakuna Mapenzi yanaumiza Maumivu yasokwisha Ulimwambia na baba Kuwa umepata bwana Sio bwana wa miraba Bwana ametulizana Leo mepata jaziba Penzi la kudanganyana Mapenzi yanaumiza Maumivu yasokwisha Hapa ninaweka kaba Nimechoka… Read more Mapenzi yanaumiza.

Kila la heri mwereni.

KILA LA HERI MWERENI Salamu zangu nawapa, kaka yenu muadhamu Niwambie pasi pupa, jambo lililo muhimu Mtihani si mfupa, kwenu usiwe mgumu Mwereni kila la heri, nawaombea Wambua Muda sasa umefika, wa kuyavuna mapando Kwa walimu sina shaka, waliwalisha uhondo Mwisho atakaye cheka, hucheka kwacho kishindo Mwereni kila la heri, nawaombea Wambua Alopanda pametosha, mwambieni aamke Atavuna pamekwisha, jina la shule lishuke Walimu wakifundisha, kaeni ange mshike Mwereni kila la heri, nawaombea Wambua Ng’ombe msham’maliza, mkia usiwashinde Mwishoni mkateleza, nawasihi chondechonde Kamwe msije kucheza, Malaika wawashinde Mwereni kila la heri,… Read more Kila la heri mwereni.

Miezi tisa baadaye.

Umbali tuloutoka,ni neema zake Bwana, Ndiyo maana nataka,shuhuda ana kwa ana, Usiwahi kunicheka, labda tulipokezana, Masikio uyatege,kigoda ukikalia. Imekuwa unoita,miezi ile ya mwambo, Fedha nazo kuzipata,limekuwa gumu jambo, Uchumi umezorota, biashara kwenda kombo. Hatima yake ni njaa, umaskini na ukame. Mauko yalokithiri, ‘masonko’ kwa mahawinde, Yameshiba makaburi,wafu wakawa washinde, Haya yote siyo siri, wala siyo peremende, Wakwetu walotuaga, tukabaki kinywa wazi. Wanaetu waliimba,wimbo usio mzuri, Wakaweza pata mimba, ambazo zimewathiri, Wazazi na wakagomba, hawakuata kiburi, Magonjwa wakapokea, ukimwi hata zinaa. Nitaikosa nidhamu, sipotaja mtalaa, Sitaki kuwa hakimu,jionee ‘navyokaa, Kila mara… Read more Miezi tisa baadaye.