Ushairi.

Huu ni sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalum fasaha na yenye muwala kwa lugha ya mkato,sitiari, picha au ishara katika maandishi, usemi au mahadhi ya wimbo ili kueleza tukio au mawazo.

Vitu vivanyounda ushairi katika kiswahili ni kama yafuatayo:

1.Takriri-hii ni mbinu ya kurudia jambo kwa madhumuni fulani.Vina na urari wa mizani ni aina ya takriri.Aidha, mshairi anaweza kurudia maneno au silabi fulani kwa dhamira maalum.

2.Taswira-hii ni mbinu ya kuunda picha ya jambo katika fikra ya msomaji/msikilizaji au utungo wenyewe.

3.Tamathali za semi-hapa ndipo tunapata mbinu mbali za lugha zinazoipamba shairi mathalani balagha,nahau, sitiari na kadhalika.

4.Hisia za kishairi-Aghalabu hutokana na msukumo wa ndani wa moyoni alio nao mshairi anapotunga shairi.Hujitokeza kupitia uteuzi na mpangilio mzuri wa maneno yanayowakilisha ujumbe husika.

5.Lugha ya mkato-Mambo huzungumzwa kwa kifupi kuliko yalivyo katika maongezi ya kawaida na hii hufaulishwa kwa kutumia tamathali badala ya maelezo.

6.Fani na maudhui-Fani hujikita katika muundo, mtindo na matumizi ya lugha ilhali maudhui ni ujumbe unaowasilishwa katika shairi.

7.Mchezo wa maneno-Hutumia kuongeza ladha katika usemaji.K.m kutumia maneno yanayofanana kidogo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s