Dhana ya Fonolojia.
Fonolojia ni taaluma inayoshughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti zinazotumika katika lugha fulani mahususi.Kiwango hiki cha lugha huchunguza uamilifu wa sauti mahususi zinazotumika katika lugha maalumu.
Kipashio cha chini kabisa cha Fonolojia ni fonimu.Fonimu ni sauti anuwai zinazotumika kuunda maneno katika lugha ya kiswahili.Aidha , kipashio hiki hutumika kutofautisha maneno ya lugha.K.m hapa na haba.
Dhima ya kwanza ya fonolojia ni kueleza na kufafanua mifanyiko mbalimbali ya kifonolojia mathalani namna sauti zinabadilika kutoka sauti moja hadi nyingine hasa tunapojenga maneno tofauti.
Kazi ya pili ni kuonyesha sifa za kiarudhi katika lugha kama vile shadda,toni,kiimbo.
Jukumu la tatu la taaluma hii ni kueleza jinsi sauti za fonimu hufuatana kujenga silabi na maneno yanayokubalika.K.m Maneno ya Kiswahili huanza kwa irabu au konsonanti lakini kila neno sharti likamilike na sauti ya voweli.Yale maneno yanayokopwa huswahilishwa ili kufuata mtindo huu.
Kazi nyingine ya fonolojia ni kuorodhesha fonimu za lugha husika.