Aina za vielezi.
Kielezi ni neno linafafanua/linapambanua kitendo/kitenzi.Hueleza kitendo kilifanyika vipi,wapi,lini na mara ngapi.
Kutokana na maelezo haya tunapata aina zifuatazo za vielezi:
- Vielezi vya wakati/njeo k.m Mgeni atawasili asubuhi.’Asubuhi’ ni kielezi cha wakati.
- Vielezi vya mahali k.m Walimu wale wanaenda shuleni.’Shuleni’ ni kielezi cha mahali.Aghalabu vielezi hivi hutamatika kwa kiambishi ‘ni’.
- Vielezi vya namna/jinsi k.m Tulitembea harakaharaka tukienda sokoni.’Harakaharaka’ ni kielezi cha namna.
- Vielezi vya idadi/kiasi k.m Mgeni yule huwa anatembelea mara kwa mara.’Mara kwa mara’ ni kielezi cha idadi.
Tanbihi:Kila aina ya kielezi huweza kuainishwa katika vikundi vingine vidogo.