Sifa Za Mhakiki.
Mhakiki huwa na sifa zifuatazo:
- Anatakiwa asikuwe mpondaji wa kazi ya watu wengine; asichukue au kusifia tu kazi za waandishi kwa sababu zake binafsi bila ya kuzingatia ukweli wa kazi hiyo.
- Mhakiki anastahiki awe amesoma kazi mbalimbali za fasihi na sio tu ile anayoifanyia uhakiki ili awe na ujuzi zaidi katika uwanja wa uhakiki.
- Mhakiki anatakiwa asome tahakiki za wahakiki wengine katika uwanja wa fasihi hata nje ya jamii ili kupata upanuzi zaidi katika kazi ya uhakiki.
- Mhakiki anastahiki aelewe historia na siasa ya jamii inayohusika.Hili litamwezesha kuelewa matatizo ya jamii hiyo.
- Mhakiki anatakiwa ajue historia na mazingira yaliyomkuza mwandishi.