Matumizi Ya ‘Kwa’.
‘Kwa’ hutumika kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo:
- Kuonyesha dhana ya pamoja na .K.m Wasichana kwa wavulana walihudhuria mkutano.
- Kuonyesha kifaa au chombo kilichotumika.K.m Fundi alichota changarawe kwa sepetu.
- Kuonyesha akisami.K.m Yeye alizoa alama tisa kwa kumi.
- Kuonyesha uhusiano kati ya mtu/watu na mahali.K.m Nitaenda kwa mwalimu kumtembelea.
- ‘Kwa’ ya A-unganifu.K.m Kuimba kwa wanafunzi kuwafurahisha walimu.
- Kuonyesha dhana ya kielezi.K.m Tulimkaribisha mgeni kwa mkono mkunjufu.
- ‘Kwa’ ya Kiulizi.K.m Kwa nini umechelewa kuja darasani?
- Kwa kumiliki ya nafasi ya kwanza umoja katika ngeli ya KU-KU.K.m Kucheza kwangu kulifurahisha wengi.