Aina za bahari ya mashairi.
Kuna aina mbalimbali za mashairi kwa kuzingatia kigezo cha bahari.
- Sakarani-Hili ni shairi lenye bahari zaidi ya moja.
- Ukara-Hili ambalo vina vya kipande kimoja hubadilika kutoka ubeti moja hadi mwingine ilhali vina vyaupande mmoja havibadiliki kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.
- Ukaraguni-Hili ni shairi ambalo vina vya kati na vile vya mwisho hubadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.
- Kikwamba-Hili ni shairi ambalo neno au kifungu cha maneno hurudiwarudiwa ili kutanguliza mshororo au ubeti unaofuata.
- Mtiririko-Hili ni shairi ambalo vina vya kati vya mwisho havibadiliki kutoka ubeti wa kwanza hadi ule wa mwisho.
- Mathnawi-Hili ni shairi ambalo lina vipande viwili yaani ukwapi na utao.
- Ukawafi-Hili ni shairi ambalo lina vipande vitatu yaani ukwapi,utao na mwandamizi.
- Ngojera-Hili ni shairi la majibizano kati ya watu wawili.
- Madhuma-Hili ni shairi ambalo kipande kimoja hutoa swali na kipande kingine hutoa jawabu.
- Sabilia-Hili ni shairi lisilokuwa na kibwagizo.
- Msuko-Hili ni shairi ambalo mshororo wake wa mwisho ni mfupi kuliko mishororo ya awali.
- Pindu/Mkufu/Nyoka- Hili ni shairi ambalo neno la mwisho/Kifungu cha maneno cha mwisho katika kila ubeti hutumika kuanza ubeti ufuatao.
- Utenzi-Hili ni shairi ambalo ni ndefu na lina kipande kimoja katika kila ubeti.