Aina za mashairi.
Kuna aina mbalimbali za mashairi kwa kuzingatia kigezo cha mishororo.
- Tathmina-Hili ni shairi lenye mshororo mmoja katika kila ubeti.
- Tathnia-Hili ni shairi lenye mishororo miwili katika kila ubeti.
- Tathlitha-Hili ni shairi lenye mishororo mitatu katika kila ubeti.
- Tarbia-Hili shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti.
- Takhmisa-Hili ni shairi lenye mishororo tano katika kila ubeti.
- Tasdisa-Hili ni shairi lenye mishororo sita katika kila ubeti.
- Usaba-Hili ni shairi lenye mishororo saba katika kila ubeti.
- Unane-Shairi lenye mishororo minane katika kila ubeti.
- Utisa-Shairi lenye mishororo tisa katika kila ubeti.
- Ukumi-Shairi lenye mishororo kumi katika kila ubeti.