Msamiati wa watu na kazi zao.
Watu katika jamii wana taaluma au kazi mbalimbali wanapopata posho na riziki zao.
- Mhasibu-Huyu ni mtu anayeweka rekodi za matumizi ya pesa.
- Sogora-Huyu ni fundi wa kupiga ngoma.
- Ngariba-Huyu ni mtaalamu wa kupasha wavulana tohara.
- Mfawidhi-Huyu ni mtu aliyeteuliwa kuongoza shughuli katika kitengo au idara.
- Mfasiri/mkalimani/mtarujumani-Huyu ni mtu anayeeleza maelezo yaliyosemwa katika lugha moja hadi nyingine.
- Kuli-Huyu ni mtu anayefanya kazi ya kupakia na kupakua mizigo bandarini.
- Mwandisi-Huyu ni mtaalamu wa kuunda vifaa na kurekebisha vilivyoharibika.
- Mkutubi-Huyu ni mtu anayefanya kazi ya kuazima na kuhifadhi vitabu maktabani.
- Kocha-Ni mwalimu wa mchezo.K.m kandanda.
- Mpigaramli-Huyu ni anayebashiri kwa kupiga bao.
- Dalali-Mtu anayeuza bidhaa katika soko la mnada.
- Mzegazega-Mtu anayeuza maji kwa kutembeza.
- Mhadhiri-Huyu ni mwalimu wa chuo kikuu.
- Nokoa/mnyapara-Mtu anayesimamia watu wanaofanya kazi shambani.
- Hakimu-Mtu anayeamua kesi mahakamani.Pia huitwa jaji.
- Mnajimu-Mtu mwenye elimu ya nyota.
- Dobi-Mtu anayefua na kupiga pasi nguo za watu wengine kwa malipo.
- Chura-Mtu anayefagia na kuzoa taka chooni au barabarani.
- Tarishi/Katikiro-Mtu anayeajiriwa ofisini ili kutoa huduma ya kupeleka barua au ujumbe.
- Utingo/taniboi-Mtu anayekusanya nauli kwenye basi au matatu.
- Mkufunzi-Mwalimu wa chuo cha ualimu au diploma.
- Mwashi-Mtu ajengaye vyumba kwa kutumia mawe.
- Mhunzi-Mtu anayefua/kutengeneza vifaa vya madini kama vile vyuma.
- Msarifu-Mtu mwenye mamlaka ya kusimamia,kutunza na kuidhinisha matumizi ya fedha katika taasisi au asasi maalum.
- Rubani-Anayeendesha ndege.