Salamu za Kiswahili.
Katika lugha ya Kiswahili kuna jinsi husubahiana na kujuliana hali.Aghalabu hutegemea wakati unapotumika na wahusika kuzingatia kigezo cha umri.Baadhi ya salamu za Kiswahili ni kama zifuatazo.
- Alamsiki-Hii salamu hutumika usiku wakati mmoja anaaga mwengine.Jawabu ni binuru.
- Salaam aleikum-Hii ni salamu inayotumika wakati wowote na baina ya mtu yeyote na mwengine.Jawabu ni aleikum salaam.
- Hujambo-Hii pia hutumika wakati wowote na baina ya mtu yeyote na mwengine.Jawabu ni sijambo.
- Cheichei-Hii hutumika mara nyingi na watu wenye umri uliokaribiana (mariika). Hutumika wakati wowote.Jawabu ni ewaa.
- Sabalkheri-Hutumika baina ya mtu mkubwa na mtu mwingine mkubwa majira ya asubuhi.Jawabu ni alkheri.
- Masalkheri-Hutumika pia baina ya watu wakubwa majira ya jioni.Jawabu ni alkheri.
- Shikamoo-Hii ni salamu itumikayo baina ya mtu mdogo na mtu mkubwa kwa umri.Hutumika wakati mtu amekutana mwingine kwa mara ya kwanza siku hiyo.Jawabu ni marahaba.
- Habari-Hii hutumika wakati wowote.Jawabu ni nzuri/njema.