Dhana Ya Jamii Lugha.

Kwa mujibu wa Mekacha (2011) dhana ya jamii lugha imetafsiriwa kwa mitazamo mbalimbali, hata hivyo wataalamu wengi wanakubaliana na maana ya jumla kuwa jamii lugha ni watumiaji wa lugha wanaoishi katika eneo moja ambao hubainishwa kwa mahusiano yao ya kuendelea kutumia aina fulani ya lugha tofauti na watumiaji wengine wa lugha hiyohiyo. Licha ya fasili hii kuonekana kuwa ni rahisi kueleweka, bado ina utata katika kupata data wakati wa uainishaji wa wazungumzaji wake na uchanganuzi wa data za isimujamii. Utata huu unajibainisha katika mambo yafuatayo;i. Kujua mahali ambapo mipaka ya watumiaji wa lugha inaanzia na kuishia na kama inawezekana kukawa na mipaka ya eneo moja la jamii lugha isiyoingiliana na mipaka ya eneo lingine
ii. Uwezekano wa wazungumzaji wa lugha katika jamii lugha moja, kuzungumza lugha moja au zaidi. Je, wanatumia lahaja, lugha sanifu, misimu, lafudhi au wanatumia lugha zote?
iii. Vigezo vinavyotumika kuwabaini au kuwaainisha watumiaji wanaopatikana katika jamii lugha moja na kuwafanya waonekane kuwa wa jamiilugha husika.Maswali haya na mengine mengi yanaifanya tafsiri ya dhana ya jamiilugha ionekane kuwa ni tata kinadharia na kiutendaji. Tutatumia misingi mitatu ili kuifahamu dhana ya jamiilugha:i. Msingi wa kutumia lugha
Imezoeleka katika jamii nyingi lugha kutumika kama nembo ya jamii fulani ambapo watu wanaotoka au wanaopatikana katika jamii fulani hutambulishwa kwa lugha yao. Mfano tunaweza kupata lugha ya Kiswahili (Waswahili), Kichaga (Wachaga), Kiingereza (Waingereza), Kijaluo (Wajaluo), Kikalenji (Wakalenji) nakadhalika.Katika utambulisho huu jamii au taifa linalotumia lugha moja ndilo linalopewa lugha moja. Kunapokuwa na matumizi ya lugha zaidi ya moja taifa au jamii husika haitambulishwi kwa Lugha, kwa mfano hutuwezi kuwa na jamiilugha ya Watanzania, Wakenya, Waghana nakadhalika. Jamii hizi huwa ni muktadha halisi wa matumizi ya lugha na si mtu mmojammoja kwa vile lugha ni mali ya jamii.Hii ni kusema, Jamiilugha hujidhihirisha katika mawasiliano ambayo hufanikiwa katika misingi ifuatayo;
 Kuelewana kwa wazungumzaji wa lugha miongoni mwao kunatokana na wazungumzaji wenyewe kuwa ni zao la jamii moja
 Watumiaji wa jamiilugha moja huelewana kiurahisi kwakuwa wanazielewa kanuni na taratibu za mawasiliano zinazotumiwa na watumiaji lugha wote
 Wazungumzaji wa lugha hiyo huwa na ujuzi na uzoefu wa muda mrefu wa kutumia lugha hiyo kwa nia ya kurithishana.Kwa mantiki hii, lugha ndio inayojiwekea mipaka ya jamiilugha. Mipaka huanzia na kuishia mahali lugha inapoishia. Tatizo la mtazamo huu ni kuwa kwanza, kuwepo kwa baadhi ya watu kuanza kutumia lahaja tofauti, Pili kunakuwa na matumizi ya lugha zaidi ya moja na hivyo kuwa vigumu kupata jamiilugha kirahisi kwasababu kunapotokea jamii zaidi ya moja kila jamii hujiona bora kuliko nyingine.ii. Msingi wa kutumia mahali/Eneo
Watu wanaounda jamiilugha moja wanakaa katika eneo moja lenye mipaka mahsusi ya kijeografia. Wanassosholojia hutumia msingi wa mahali katika kubaini jamiilugha. Huamini katika msingi kuwa, watu wanapokuwa katika eneo moja kwa muda mrefu hujiundia kanuni na taratibu zao za namna ya kuishi, yaani mila na desturi. Watu hawa hujiwekea mipaka yao ili kujitofautisha na jamii nyingine, mipaka hii yawezakuwa milima, mabonde, mito, misitu minene nakadhalika. Mipaka hii ya kijeografia huheshimiwa daima na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Hivyo, ili kujua jamiilugha wataalamu wa lugha hawana budi kutumia misingi ya mahali mahali na lugha kuibaini jamiilugha kwakuwa ni vitu vinavyotegrmeana na kukamilishana.iii. Msingi wa makubaliano wa kimazoea.
Ni msingi unaohusu jamiilugha ndogondogo ndani ya jamiilugha kubwa katika eneo fulani. Jamiilugha hizi zaweza kuwa za wafanyakazi wa kampuni fulani, wanafunzi, wanachuo, wafanyabiashara, vijana, jinsia fulani nk. Msingi wa makubaliano ya usemaji unatokana na mazoea ya muda mrefu kutokana na kuwa pamoja katika shughuli au mahali fulani. Tatizo la jamiilugha za aina hii ni utata katika kupata idadi halisi ya jamiilugha kutokana na kukosa ukomo. Hii inatokana na ukosefu wa mipaka dhahiri ya jamiilugha moja na nyingine kwa kuwa mtu mmoja anaweza kujibainisha katika jamiilugha zaidi ya moja. Mfano, mtu kuwa mfanyabiashara, mwanafunzi na vilevile mfanyakazi wa bandarini. Msingi huu unaelekea kuwa si imara.MAKUNDI YA JAMIILUGHA1. Jamiilugha zinazotumia lugha moja
Ikiwa jamiilugha inatumia lugha moja, basi jamiilugha hiyo inasemekana kuwa yenye kutumia lugha moja (Monolingual speech community). Lugha hii hutumika katika maeneo yote ya matumiazi ya lugha, maeneo rasmi ya utawala na serikali na yasiyo rasmi ya matumizi ya lugha kama vile majumbani katika kiwango cha familia na mtu na mtu. Wanajamii wote wandhaniwa kuielewa na kuitumia lugha husika kiufasaha katika shughuli zao za kila siku.Hata hivyo, katika karne ya leo ambapo kuna maingiliano na mawasiliano bora zaidi mingoni mwa wanajamii duniani ni vigumu kupata jamiilugha yenye kutumia lugha moja tu katika mawasiliano yake. Ugumu huu unatokana na maingiliano kupitia njia mbalimbali kama uhamiaji, utalii, elimu, dini, ndoa, ukimbizi, mawasiliano ya kimtandao nk.Vilevile hata katika jamiilugha yenye kutumia lugha moja bado kunaweza kutokea suala la tofauti za kilahaja. Kwa upande mwingine watumiaji lugha wa mipakani hulazimika kujifunza lugha nyingine zaidi kutokana maingiliano ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni na watu kutoka katika jamiilugha wanayopakana nayo. Hii inawafanya wawe na lugha mbili tofauti (jamiilugha uwili) kwa wakati mmoja..Kimsingi dhana ya jamiilugha inayotumia lugha mojailikuwepo kwa Tanzania kabla ya ujio wa wakoloni ambapo kila jamii ilitumia lugha moja. Hivyo, kulikuwa na taifa la wahehe, wachaga, wasukuma nk. Baada ya ujio wa wakoloni mataifa asilia yakawa chini ya utawala mmoja. hivyo kukawa na mataifa makubwa zaidi kama ya Kenya, Tanzania na Uganda. Hapo ndipo muingiliano ukawa mpana zaidi.2. Jamiilugha Uwili
Ikitokea katika jamii kuwa na matumizi ya lugha mbili kwa wakati mmoja tunaweza kusema jamii husika ni jamiilugha uwili. Kigezo kinachotumika ni idadi ya lugha zinazotumika. Inawezekana kupata jamiilugha uwili katika mazingira ya Tanzania ambapo watu wanaweza kuzungumza lugha ya Kiswahili na wakati huohuo wanazungumza lugha mojawapo kati ya lugha za asili. Hata hivyo, kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, mtu mmojammoja wanajua lugha zaidi ya mbili. Kiswahili, Kiingereza/ Kifaransa, Lugha ya/za asili nk.3. Jamiilugha Ulumbi
Katika mzingira ya kawaida kwa watanzania kuna wakati wazungumzaji humudu lugha zaidi ya mbili. Mfano, mtu anaweza kuzungungumza lugha moja au zaidi kati ya lugha za asili, Kiswahili na lugha moja au zaidi. Mfano, anaweza kujua lugha ya Kinyakyusa, Kisafwa, Kiswahili na Kiingereza hivyo kujua lugha nne. Mwingine anaweza kujua lugha moja ya asili mfano Kisukuma, Kigogo na Kiswahili tu na akawa anajua lugha tatu nk. Hivyo, idadi ya lugha katika jamiilugha ulumbi hutofautiana kati ya mtu na mtu na jamiilugha na jamiilugha. Vilevile ikumbukwe kuwa kiwango cha umahiri katika lugha anazojua mzungumzaji si lazima kiwe sawa. Kuna atamudu vizuri zaidi lugha fulani ikilinganishwa na nyingine.Sababu za Kutokea Ulumbi
Ulumbi katika jamiilugha inasemekana kuwa unasababishwa na mambo ya ndani ya jamii yenyewe na mambo yanayotoka nje ya jamii. Kwa ujumla mambo hayo ni pamoja na uhamiaji, ukimbizi, ukoloni, biashara, elimu, dini, mipaka ya kimataifa, Nguvu za dola, teknolojia ya habari na mawasiliano, nguvu [kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni] nk. Ieleweke kwamba sababu za kutokea kwa ulumbi hutofautiana kati ya jamii na jamii na msemaji mmoja na mwingine.Matatizo ya Jamiilugha Ulumbi
Tatizo la kuteua lugha ya kutumia kitaifa kati ya lugha zinazotumika. Mfano, kupata lugha ya taifa, lugha ya kufundishia na lugha rasmi. Kila jamiilugha inaweza kuwa na nguvu kimatumizi au kwa idadi ya wazungumzaji kiasi cha kutaka kuteuliwa na hivyo kuwa vigumu kupata lugha kiurahisi.Hata hivyo, inashauriwa kuwa uteuzi wa lugha kitaifa unapaswa kufanyika kwa uangalifu sana kwa kushirikisha makundi mbalimbali ya kijamii ili kuepuka minyukano ya kimaslahi miongoni mwa wanajamii.Vilevile ulumbi unaweza kusababisha ukosefu wa umoja na mshikamano miongoni mwa wanajamii kwa vile kunakuwa jamii zinazojibainisha katika lugha na kila jamii inakuwa na utamaduni wake na hata mazingira yake.MATUMIZI YA LUGHA
Katika kipengele hiki tunatarajia kuchunguza jinsi matumizi ya lugha yanavyojibainisha miongoni mwa watumialugha na jamiilugha. Ni kwa nini lugha hutumika tofautitofauti kati ya jamii moja na nyingine.Sababu za kutofautiana kwa matumizi ya lugha:
Umri, elimu, jinsia, dini, matabaka [kisiasa, kiuchumi, kijamii], makabila, jiografia, nk.Makundi ya lugha za Tanzania
Tanzania ni nchi inayoonekana kama eneo la makutano ya makundi ya lugha za asili katika Bara la Afrika. Makundi haya ni Naija-Kongo (Bantu), Nailosahara, Afroasia (kikushitiki) na Kikhoisani. Haya ni makundi ya msingi.Nailosahara
Ni kundi lingine la lugha ambalo asili yake ni Afrika ya Kaskazini Misri, Ethiopia na Sudani. Mfano wa lugha za kundi hili Tanzania ni KimasaiAfro-Asia
Ni kundi kubwa lilizaa kundi la kushiti ambalo linajumuisha lugha kama Iraqw[kimbulu] 500,000 na lugha nyingine za Burunge, Alangwa,Gorowa na Ma’a (Mbugu) zina jumla ya wazungumzaji 40,000. Sifa moja kubwa ya lugha hizi ni sauti ya mkwaruzo kooni inayodhihirisha kuwa asili yake ni Uarabuni.Khoisani
Asili yake ni Afrika kusini. Mfano wa lugha TZ ni Kisandawe na Kihazabe . Sifa kubwa ya lugha hii ni konsonanti za kukisi.Bantu
Hili ni kundi linatokana na kundi la Benue Kongo ambalo lilitokana na kundi la Naija-kongo.Kundi hili linalojumuisha lugha nyingi zaidi pamoja wa wazungumzaji nchini Tanzania. Linahusisha lugha kama vile Kisukuma, kichaga, kinyakyusa, kiha nk.
Pamoja na kuwepo kwa makundi haya, bado kuna matumizi ya lugha nyingine za kigeni kama vile Kingereza, Kilatini, Kiarabu, Kifaransa, nk ingawa kwa viwango vidogo.Diaglosia
Katika jamii hutokea wakati mwingine lugha mbili kutumika, moja kutumika matika mazungumzo ya kawaida katika familia, mtu na mtu wakati lugha nyingine hutumika katika shughuri lasmi kama elimu mahakama, biashara, bunge nk. Vilevile inaweza kutokea lugha moja kuwa na lahaja tofauti ambapo kunakuwa na lahaja ambayo inatumika katika mawasiliano ya kawaida ilihali lahaja nyingine hutumika katika mawasiliano rasmi. Lugha ua lahaja inayotumika katika mawasiliano ya kawaida hupewa mhadhi ndogo C na inayopewa matumizi katika shughuri rasmi hupewa hadhi ya juu J. kunapokuwa na mahusiano ya namna hii tunasema kuna Diaglosia (kifaransa “diglossie”).MAMBO YANAYOJIPAMBANUA KATIKA DIAGLOSIAa. Uamilifu
Lugha au lahaja J hutumika zaidi ikilinganishwa na lugha au lahaja C. Hii inatokana na kupewa majukumu mengi zaidi mfano kaika elimu, mahakama, biashara, dini, mahusiano ya kimataifa nk. Ni lugha inayoeleweka na kutumika na watu wengi zaidi ikilinganishwa na lugha ua lahaja C. Wageni wanapotaka kujifunza hupenda kujifunza lugha J. Vilevile maarifa mengi huwa katika Lugha au lahaja J ingawa ufafanuzi wake waweza kufanyika katika lugha au lahaja C.b. Umaarufu
Watumiaji wa lugha huiona lugha au lahaja J kuwa ni bora na maarufu zaidi kuliko C. Matokeo yake watu wengi zaidi hujifunza na kutumia J. mfano, watu watataka kusikiliza nyimbo, filamu, mashairi katika J hata kama hawaelewi ilikinganishwa na katika C. Vilevile katika dini lugha C hutumika zaidi. Mfano Kiarabu, Kiswahili nk.c. Mapokeo katika maandishi
Jamii huamini kuwa lugha iliyo katika maandishi ndiyo kiwakilisho sahihi cha lugha J. Hata tabaka la watumia lugha J huamini hivyo. Matokeo yake lugha J hutukuzwa wakati C hupuuzwa. J yaweza kuwa ya kizazi kilichopita au kilichopo mfano mashairi, dini, falsafa, sheria, sayansi nk.d. Ujifunzaji Lugha
Katika kiwangoi cha familia watu hutumia lugha C. Watoto wanapowasiliana wao kwa wao au na wazazi hutumia Lugha C. Hata hivyo, katika shughuri rasmi kama vile elimu, mahakama, redioni lugha J hutumika. Kanuni na miiko ya sarufi ya lugha J hufundishwa darasani wakati lugha C hufundishwa kimapokeo/kwa kurithishwa.e. Usanifishaji
Lugha J imefanyiwa tafiti nyingi zaidi kuhusu sarufi, msamiati, mitindo, otografia nk na miiko yake.Matokeo yake Lugha J inakuwa imesanifishwa na otografia yake haibadiliki ingawa maana yaweza kubadilika katika muktadha fulani.f. Msamiati
Kunakuwa na mwingiliano mkubwa wa msamiati kati ya lugha J na C. Hata hivyo, lugha J ina msamiati mwingi zaidi wa kiufundi na kigeni ambao unakosa visawe katika J. Vilevile msamiati katika lugha C mwingi sio rasmi. Kwa mifano;
Mother mum
Cigarette fag
Police officer cop
Steal pinch
Children kidsg. Sarufi
Sarufi ya lugha J imechanganuliwa zaidi na kuandikwa wakati sarufi ya lugha C ni mara chache kuandikwa kwa vile huchukuliwa kuwa ni hafifu.Mambo yanayoweza kusababisha diglosia kutokea
a. Kuwepo lugha zaidi ya moja au kutokea kwa lahaja nyingi katika lugha.
b. Kuwepo kwa matabaka katika jamii. Tabaka lenye nguvu kisiasa, kiuchumi litaathiri uteuzi wa lugha J.

1 Comment »

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s