Sifa za Fonimu.
Fonimu ina sifa zifuatazo:
- Kila fonimu ina sifa zake za kifonolojia zinazoonesha uamilifu wa fonimu hiyo katika lugha maalumu.
- Kila fonimu hushiriki kikamilifu katika ujenzi wa maneno na kutofautisha maneno yenyewe.
- Fonimu moja haina maana kwa kuwa si kiashiria cha kiashiriwa chochote.
- Ukibadili fonimu moja katika neno basi maana ya neno hilo itabadilika.
- Kila fonimu ina sifa zake za kifonetiki zinazoweza kuelezwa na kufafanua fonimu hiyo.
- Kila lugha ina fonimu zake na fonimu hizo hazifanani katika uamilifu wake.
- Ukipunguza fonimu katika neno maana ya neno hilo itabadilika au kupotea kabisa.
- Ukipangua mpangilio wa fonimu katika neno maana ya neno hilo itabadilika au kupotea.
- Ukiongeza fonimu katika neno maana ya neno hilo itabadilika au kupotea.
- Sifa zote za fonimu za lugha maalum huelezwa na watumiaji wa lugha hiyo ikiwa ni sehemu ya umilisi wa lugha yao.