Skip to content

Month: September 2020

Nifundishe wafundishike.

NIFUNDISHE WAFUNDISHIKE Moyoni siweki koma, imekita ndoto yangu Ama kweli ninatama, nishaweka roho yangu Ukufunzi kazi njema, saidia Mungu wangu Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike Wawe nao marubani, wapae kwenye anga Waipasi mitihani, wasikose ule unga Ujinga hapo shuleni, waupige ile chenga Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike Wakafike Marekani, waitwe nao wasomi Wazunguke uzunguni, wazishike zao ndimi Warudi hapa melini, wasalimu hata nami Ndoto yangu ukufunzi fundishe wafundishike Uandishi waushike, kazi yao iwe bora Kwa riwaya wasifike, mashairi yawe bora Yamkini watajike, kama yule Walibora Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike… Read more Nifundishe wafundishike.

Nifundishe wafundishike.

NIFUNDISHE WAFUNDISHIKE Moyoni siweki koma, imekita ndoto yangu Ama kweli ninatama, nishaweka roho yangu Ukufunzi kazi njema, saidia Mungu wangu Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike Wawe nao marubani, wapae kwenye anga Waipasi mitihani, wasikose ule unga Ujinga hapo shuleni, waupige ile chenga Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike Wakafike Marekani, waitwe nao wasomi Wazunguke uzunguni, wazishike zao ndimi Warudi hapa melini, wasalimu hata nami Ndoto yangu ukufunzi fundishe wafundishike Uandishi waushike, kazi yao iwe bora Kwa riwaya wasifike, mashairi yawe bora Yamkini watajike, kama yule Walibora Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike… Read more Nifundishe wafundishike.

Nahau na maana zake

1.Amekula chumvi nyingi=ameishi miaka. mingi 2,Ana mkono wa birika=mtu mchoyo 3.Ametutupa mkono=amefariki,amekufa 4.Ameaga dunia=amekufa,amefariki 5.Amevaa miwani=amelewa 6.Amepiga kite=amependeza 7.Amepata jiko=kaoa 8.Amefumgapinguzamaisha=ameolewa 9.Anawalanda wazazi wake= kawafanana wazazi wake kwa sura 10.Kawachukua wazazi wake=anafanana na wazazi wake kwa sura na tabia. 11.Kawabeba wazazi wake=anawajali na kuwatunza wazazi wake. 12.Chemshabongo=fikiri kwa makini na haraka. 13.Amekuwa toinyo=hanapua. 14.Amekuwa popo=amekuwa kigeugeu 15.Ahadi ni deni=timiza ahadi yako 16.Amewachukua wazee wake= anawatunza vizuri wazazi 17.Amekuwa mwalimu=yu msemaji sana 18.Amemwaga unga=amefukuzwa kazi 19..Anaulimuwaupanga=anamaneno makali 20.Ameongeza unga=mepandacheo 21.Agiziarisasi=pigarisasi 22.Kuchungulia kaburi=kunusurika kifo 23..Fyatamkia=nyamaza kimya 24.Fimbo zimemwota mgongoni=ana alama za mapigo… Read more Nahau na maana zake

Umalenga ni basi.

UMALENGA NI BASI Moyo wangu umegoma, kutunga tena sidhani Ushairi nauhama, malenga sina thamani Bongo nalo limekwama, tungo hawazitamani Naitupa mishororo, bora nifanye muziki Yani kote makundini, tungo zangu hazisomwi Hata kule ulingoni, japo ya mbwa siamwi Kule kwetu kisimani, naliwa na langu zimwi Naitupa mishororo, bora nifanye muziki Mzee mpenda watu, hanioni mie kwani Nazimaliza sapatu, kumfata kikashani Kwake sisikiki katu, hanipi ‘ta tumaini Naitupa mishororo, bora nifanye muziki Yule mhindi wa pwani, makundini simuoni Hivi yuwapi jamani, Raneti aniauni Azitupe ‘ko hewani, nisikike redioni Naitupa mishororo, bora nifanye… Read more Umalenga ni basi.

Visawe na maana zake.

Visawe ni maneno yenye maana sawa. *Neno=Kisawe* 1. Ardhi=Dunia 2.Ari=Nia 3.Aibu=Soni 4.Azma=Makusudio 5.Binti=Msichana 6.Chakula=Mlo 7.Chanzo=Sababu 8.Cheti=Hati 9.Chuana=Shindana 10.Chubua=Chuna 11.Chubuko=Jeraha 12.Chumvi=Munyu 13.Duara=Mviringo 14.Dunia=Ulimwengu 15.Familia=Kaya 16.Fedha=Hela/Pesa 17.Fukara=Maskini 18.Gari Moshi=Treni 19.Ghasia=Fujo 20.Ghiliba=Hila 21.Godoro=Tandiko 22.Hitimaye=Mwishowe 23.Herufi=Hati 24.Hesabu=Hisabati 25.Hodari=Bingwa 26.Idhini=Ruhusa 27.Jogoo=Jimbi 28.Jokofu=Friji 29.Kandanda=Soka 30.Kenda=Tisa 31.Kichaa=Mwendawazimu 32.Kileo=Pombe 33.Kimada=Hawara 34.Kiranja=Kiongozi 35.Kivumbi=Fujo 36.Kopoa=Zaa 37.Kongoro=Gema 38.Labda=Huenda 39.Labeka!=Abee!/Naam! 40.Laghai=Danganya 41.Lisanj=Ulimi 42.Majira=Wakati 43.Manii=Shahawa 44.Masalia=Mabaki 45.Mashaka=Tabu 46.Mbio=Kasi 47.Mchoyo=Bahili 48.Mdomo=Kinywa 49.Mlolongo=Foleni 50.Motokaa=Gari 51.Msimu=Majira 52.Mtima=Moyo 53.Mtindi=Maziwa Mgando 54.Mtindo=Staili 55.Mtu=Binadamu 56.Muda=Wakati 57.Mvuli=Mvulana 58.Nahodha=Kapteni 59.Nakshi=Urembo 60.Ndoa=Chuo 61.Ndondi=Masumbwi 62.Ndovu=Tembo 63.Nguo=Mavazi 64.Nguzo=Kanuni 65.Nia=Lengo 66.Nuru=Mng’ao 67.Nyanya=Bibi 68.Nyati=Mbogo 69.Ongea=Sema/Zungumza 70.Pombe=Mtindi 71.Raba=Kifutio 72.Rabana=Mola 73.Rafiki=Sahibu/Swahibu 74.Rehani=Poni 75.Rubani=Kapteni 76.Rundika=Tufika 77.Rushwa=Hongo 78.Saka=Winda 79.Sala=Dua 80.Samani=Fanicha… Read more Visawe na maana zake.

Wasomi nchini nafasi zenu ni nini?

Salamu ziloyakini, wajumbe tusikizeni, Tubebazo kwa makini, tunataka wajuzeni, Mengi tumeyabaini, nanyi tuwaulizeni, Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini? Umma wawasubirini, toka huko mitaani Asilimia tisini, watetezi mu njiani, Vipi hamujiamini, na kujishusha thamani, Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini? Enyi wasomi nchini, nawaeleza bayani, Tuikamateni dini, tuepuke ushetani, Hapo tutajaaini, na kujua kiundani, Kwamba wasomi nchini, nafasi zenu ni nini? Jamii inatamani, ile elimu auni, Kuondolewa gizani, kuepuka hali duni, Tusiwepo mashakani, mutupunguze huzuni, Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini? Jama! tuelimisheni, watu waache uhuni, Dhima… Read more Wasomi nchini nafasi zenu ni nini?