Mashairi Bomba.

SHAIRI: KUMBE NI……
MTUNZI: FAM

Sikuwa na wasiwasi, katika yangu safari, naeleza
Sikutaka mfuwasi, wala sikupanda gari, sikiliza
Sikupenda kujighasi, sikuifanya kikiri, sikuweza
Nilikwenda polepole

Njia nikaiandama, sio ya barabarani, nawambia
Popote sikusimama, japo yekuwa mwituni, mwasikia
Khofu kwangu ikahama, hatembea kwa amani, sehofia
Sikuogopa chochote

Kwa mbali nikasikia, sauti iliyo kali, inanita
Huku kwato zanijia, zimekazana kwa kweli, sikusita
Na wala sikukimbia, nikenda bila kujali, kwatakwata
Njia nikaiandama

Nilipofika kwa mbele, wallahi sikuamini, sikioni
Nesikia makelele, yasema Mimi ni jini, maluuni,
Metumwa nije nikule, kafara ya kijijini, huamini?
Moyo ukaanza khofu

Nyuma nilipogeuka, roho yekwenda mbinguni, mara moja
Neona bonge la joka, linavichwa sabiini, linakuja
Vizuri likanishika, likanitia kinywani, halengoja
Ghafula nikashituka

(Mpemba Orijinali)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s