Nifundishe wafundishike.

NIFUNDISHE WAFUNDISHIKE

Moyoni siweki koma, imekita ndoto yangu
Ama kweli ninatama, nishaweka roho yangu
Ukufunzi kazi njema, saidia Mungu wangu
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

Wawe nao marubani, wapae kwenye anga
Waipasi mitihani, wasikose ule unga
Ujinga hapo shuleni, waupige ile chenga
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

Wakafike Marekani, waitwe nao wasomi
Wazunguke uzunguni, wazishike zao ndimi
Warudi hapa melini, wasalimu hata nami
Ndoto yangu ukufunzi fundishe wafundishike

Uandishi waushike, kazi yao iwe bora
Kwa riwaya wasifike, mashairi yawe bora
Yamkini watajike, kama yule Walibora
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

Natamani watajike, ili nami nitajike
Huko mbali wakafike, mimi naye nisifike
Pale pote wakumbuke, niliwapa hiyo fuke
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

(Akongo Kevin-Malenga)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s