Laisha vipi godoro.
Laisha vipi godoro
1. Swali naliwauliza,wakulijibu ni nani
Sikizeni miujiza,ajabu lokitandani
Alinijuza ajuza,fumbo hili lafumbwani
Laisha vipi godoro,mwili ukagusa chaga
2. Laisha vipi godoro,ingali ni haliliwi
Laisha vipi godoro,nalo ni kama liduwi
Laisha vipi godoro,ajabuye halistawi
Laisha vipi godoro,adi lakuwa usawa
3. Laisha vipi godoro,jawabu hapa nipeni
Laisha vipi godoro,fumbo kwenu mafanani
Laisha vipi godoro,naenda kama utani
Laisha vipi godoro,tamati nilala tani
Duwi : Samaki mwenye gamba gumu
(Abuuabdilah-Malenga)