Lazima ya Barakoa.

LAZIMA YA BARAKOA.

Hodi hodi ndugu zangu, leo nimerudi Tena.
Sana nashkuru Mungu, sijapatwa na korona.
Mvipi nanyi wenzangu, hali zenu mwaziona.
Lazima ya barakoa, sasa imerudi tena.

Wana nchi sikizeni, haya ninayo yanena.
Barakoa tuvaeni, tuiepuke korona.
Mzaha tusifanye, tukangoja la kuona.
Lazima ya barakoa sasa imerudi tena.

Amri imeshatoka, ifanywe oparesheni.
Polisi watakushika, na wakutoze faini.
Faini wanayotaka, ni ELIFU ISHIRINI.
Lazima ya barakoa, sasa imerudi tena.

Tulidhani imekwisha, barakoa kazitupa.
Sheria tukakatisha, tukaanza kuzikwepa.
Sasa imejirudisha, tena merudi kwa pupa.
Lazima ya barakoa, sasa imerudi tena.

(Mtunzi:Mohammed Dzugwe)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s