Bebi Rudi Nyumbani.

(1) Shairi nakwandikia, matozi yakinitoka, Meshindwa kuyazuia, ja maji yabubujika, Rudi wangu maridhia, mwana wetu asumbuka, 𝑨𝒍𝒊𝒂 𝒏𝒂𝒎𝒊 𝒏𝒂𝒍𝒊𝒂, 𝒏𝒋𝒐𝒐𝒔𝒊𝒎𝒖 𝒖𝒕𝒂𝒕𝒖𝒕𝒖𝒍𝒊𝒛𝒂.

(2) Si usiku si mchana, alia bila kuchoka, Usingizi kamwe hana, nyumbani siwezi toka, Kucheka hacheki tena, naomba uje haraka, 𝑲𝒂𝒛𝒊 𝒛𝒂𝒏𝒊𝒍𝒆𝒎𝒆𝒂, 𝒏𝒋𝒐𝒐 𝒖𝒏𝒊𝒔𝒂𝒊𝒅𝒊𝒆.

(3) Nipo jikoni napika, naye yupo mgongoni, Alia akitapika, sijui nimpe nini! Bebi nimetaabika, naomba uje nyumbani, 𝑰𝒏𝒈𝒂𝒘𝒂 𝒕𝒖𝒍𝒊𝒌𝒐𝒔𝒂𝒏𝒂, 𝒏𝒂𝒌𝒖𝒕𝒂𝒌𝒂 𝒌𝒂𝒏𝒅𝒐 𝒚𝒂𝒏𝒈𝒖.

(4) Nikimlisha chakula, kidogo anajinyea, Yabidi niache kula, maji nikayaendea, Chakula hataki kula, kinyesi akichezea, 𝑵𝒊𝒎𝒆𝒚𝒂𝒑𝒂𝒕𝒂 𝒎𝒂𝒇𝒖𝒏𝒛𝒐 , 𝒎𝒘𝒂𝒏𝒂𝒎𝒌𝒆 𝒏𝒊 𝒎𝒖𝒉𝒊𝒎𝒖

(5) Hakuna mtimilifu, njoo tusameheane, Binadamu tu dhaifu, bebi tuvumiliane, Wewe ndio yangu kufu, kubali turudiane, 𝑵𝒂𝒔𝒖𝒃𝒊𝒓𝒊 𝒋𝒊𝒃𝒖 𝒍𝒂𝒌𝒐, 𝒉𝒆𝒃𝒖 𝒑𝒊𝒈𝒂 𝒉𝒂𝒕𝒂 𝒔𝒊𝒎𝒖.

(𝐌𝐰𝐚𝐥𝐢𝐦𝐮 𝐍𝐲𝐚𝐤𝐮𝐧𝐝𝐢 𝐌𝐚𝐥𝐞𝐧𝐠𝐚 𝐓𝐞𝐦𝐛𝐨 𝐦𝐥𝐚 𝐧𝐲𝐚𝐦𝐚)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s