Tofauti kati ya sitiari na Jazanda.

Sitiari ni mbinu ya lugha ambayo hutumia ulinganisho hapo si kwa moja kwa moja. Mara nyingi sitiari hutokana na tashbihi ambayo ni ulinganisho wa moja kwa moja. Kwa mfano, baba mkali tutasema baba ni mkali kama simba (Tashbihi) na kutokana na tashbihi hii tutapata sitiari ya (Baba ni simba). Kumaanisha ni mkali.

Jazanda.
Jazanda ni mbinu ya lugha ambayo huwa na maelezo bayana ambayo huwacha taswira Fulani akilini na huwa na maana fiche. Ni sawa kusema Jazanda ni Taswira yenye maana fiche. Tukielezea namna madhari yalivyo, tuone,tusikie,tuguse,tuonje,tunuse,tuhisi…basi ni taswira…ila tukifanya vyote hivyo kwa ufiche Fulani basi inakuwa jazanda. MFANO WA JAZANDA
Wanakijiji walishirikiana sako kwa bako kuudongoa mwiba uliofanya guu kufura na furaha kugura. Hapa kuashiria kubandua uongozi mbaya. Pia, “Mara nikasikia milio ya ndege katika ukimya ule uliotawala. Mara milio ya shore, Mara ya mbayuwayu. Wasiwasi wa mwasi ulinipanda niliposikia mlio wa Bundi…Mara simu yangu ikakiriza. Mjomba wangu maututi alikuwa ame…machozi yalinidondoka…..(Hapa mlio wa bundi unatupa taswira ya bundi pamwe na kutuashiria mabaya yatatokea…..)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s