Niroge.

NIROGE
niroge na nirogeke
Kwingine nisitamani
Niroge yani niteke
Unijie na ndotoni
Niroge nisiondoke
Nibaki na wewe hani
Niroge mirogo yote
Ya bara na visiwani

Niroge hata kidigo
Kiha nacho kizaramu
Uniroge si kidogo
Nipandwe wendawazimu
Niroge hata kigogo
Na ya kibiti mizimu
Niroge mirogo yote
Ya bara na visiwani

Niroge yote mahaba
Mahaba ya mahabati
Nikikuona nashiba
Najihisi na bahati
niroge bahari saba
Na kwako nijidhatiti
Niroge mirogo yote
Ya bara na visiwani

We niroge ukitaka
Nikupende pekeako
Wengine nisijetaka
Niwaone michepuko
Niroge moyo kichaka
Unijaze penzi lako
Niroge mirogo yote
Ya bara na visiwani

Niroge nimeridhia
Metosheka penzi lako
Uniroge wangu dia
nibaki kuwa wakwako
niroge tufunge ndoa
Siutaki mchepuko
Niroge mirogo yote
Ya bara na visiwani

Niroge nipo tamati
Nimefikia mwishoni
Niroge nipande chati
Kwa wengine mi sioni
Niroge vumba vumbarati
nizaimie mapenzini
Niroge mirogo yote
Ya bara na visiwani

(MTUNZI: BINTRASOOL)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s