Mungu ana Maajabu.

utasomaje kitabu,wapo shule hujafika,
utaongeaje bubu,kwa mada husohusika,
Babake mama ni babu,mjukuu hili shika,
mungu ana maajabu,sijione umefika,

sijione umefika,alo kufa hufufuka,
mpanda ngazi hushuka,na majuto kumshika
wapo walio sifika,leo wana taabika,
mungu ana maajabu,wapende utapendeka,

wapende utapendeka,pia utasaidika,
usipo pendwa ondoka,na roho ondoa shaka,
mtegemea rabuka,daima husitirika,
mungu ana maajabu,soma utaelimika,

somo utaelimika,na bidii ipachika,
siweke mbele hufuska,kamwe hutanufaika,
Alo kutusi mcheka,ipo siku takutaka,
mungu ana maajabu,mbingu ona livoweka,

mbingu ona livoweka,bila nguzo kuzishika,
mtoto kahifadhika,mezi tisa kwa hakika,
wanyama kaja tamka,lipo zawa msifika,
mungu ana maajabu,hakuna alo mfika,

Hakuna alo mfika,awe jini malaika,
sitake kutajirika,kwa walio laanika,
ukosapo o ridhika,maisha ni patashika
mungu ana maajabu,hakuna lo kamilika,

hakuna lo kamilika,uonywapo badilika,
sipende sana kufoka,hekima itakutoka,
kwa heshima imarika,mjukuu ni pulika,
mungu ana maajabu,yaso kuwa na jawabu,

yaso kuwa na jawabu,wala hayana viraka,
vipi tembe ya zabibu,itoe tunda kulika,
tafakari yangu babu,ukingoni nimefika,
mungu ana maajabu,ya masaa na dakika,

(Malenga ni Abdallah Khamis)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s