Nilikupenda lakini.
NILIKUPENDA LAKINI😭😭
Nilikupenda lakini
Kukuacha sina budi
Ulinikaa moyoni
Sikuachi makusudi
ni mipango ya manani
Kukuacha yanibidi
Nilikupenda lakini
Sina budi kukuacha.
Nilikupenda lakini
Hakuridhia wadudi
Tuwe wote mapenzini
kama ilivyo ahadi
tumeishia njiani
japo tulijitahidi
Nilikupenda lakini
Sina budi kukuacha
Nilikupenda lakini
Nimeivunja ahadi
Kuwa nawe maishani
sitaweza kujirudi
tuachane kwa amani
chuki kwetu zisizidi
Nilikupenda lakini
Sina budi kukuacha
Nilikupenda lakini
Utapata wa kuzidi
takuweka furahani
Hatokuwa mkaidi
Utakuwa na amani
Mapenzi utafaidi
Nilikupenda lakini
Sina budi kukuacha
Nilikupenda lakini
Ninatoa redi kadi
Ninauchungu moyoni
Nashindwa stahimidi
hapa mefika mwishoni
Wa zile zangu juhudi
Nilikupenda lakini
Sina budi kukuach,a
(MTUNZI:Bintrasool)