Mwenzenu nataka mke.

Mwenzenu nataka mke
Ila ajue kutunga
Asiwe mwenye makeke
Tungo ajue zifunga
Aje ndani nimuweke
Maisha tukiyapanga
Atunge napo kughani
Ndio sifa nayotaka

Atunge napo kughani
Ndio sifa nayotaka
Pia awe na imani
Amuogope rabuka
Nikija muweka ndani
Asije kuchoropoka
Mwenzeni nataka mke
Wa pili kumuongeza

Mwenzeni nataka mke
Wa pili kumuongeza
Ni mathna mana ake
mje mkinipendeza
mje msiniepuke
maisha kwenda kuanza
Kwa yule anoridhia
Mansur nimuoe

Kwa yule atoridhia
Mansur nimuoe
ndoani kwenye ingia
Nusura nimpatie
Takutunza wangu dia
Hofu wewe uitoe
Kwake mwenye kuridhia
Anifate kikashani

Kwake mwenye kuridhia
Anifate kikashani
taratibu kufatia
Nipate kwenda nyumbani
Nimuoe wangu dia
Tukaishi kwa amani
Mimi sijali kabila
Au wapi anatoka

Mimi sijali kabila
Au wapi anatoka
hata awe mla swala
Kenge nao kadharika
Kwangu afanye tijala
Awe wangu akitaka
Popote pale alipo
Aweze kujitokeza

Nimefika kikomoni
Mwenzenu nasubiria
Nasubiri kikashani
Aje alieridhia
Ni ukweli si utani
Nimeshaiweka nia
Yoyote alo tayari
Basi mimi nimuoe

(MTUNZI:MANSOOR)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s