Kila mtu ana kwao.

***KILA MJA ANA KWAO***
**
*
Mataifa kayaumba, tupate kutambuana /
Hakuna aliye mwamba, debe shinda kwa Rabbana /
Kisiwani tumetimba, ndugu kusalimiana /
Kila mtu ana kwao, huku ndiyo kwetu sie ////
*
Yaitwa toroka uje, vyema kurudi nyumbani /
Hii raha iliyoje, furaha iso kifani /
Mabadiliko yaloje, tofauti na zamani /
Kila mtu ana kwao, huku ndiyo kwetu sie ////
*
Kila mtu na asili, lilopo chumbuko lake /
Hata akienda mbali, hasahau kulo kwake /
Town ama chaka kali, yote ya moyoni mwake /
Kila mtu ana kwao, huku ndiyo kwetu sie ////
*
#Kitoni #Jimbo na #Bweni, minazi ni dushelele /
#Bwejuu na #Mbarakuni, samaki mejaa tele/
#Shungi mbili #Mfuruni, #Tumbuji #Kirongwe #Chole /
Kila mtu ana kwao, huku ndiyo kwetu sie ////

(Malenga ni Omary)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s