Mambo yanayochangia upotovu wa kimaadili.

Karne ya ishirini na moja imeshuhudia ongezeko la visa vya upotovu wa kimaadili miongoni mwa vijana na watoto.Hili limejitokeza kupitia ukahaba, usambazaji wa video za ngono,mimba za mapema, makundi ya kigaidi, migogoro ya kifamilia miongoni mwa nyingine.

Chanzo cha vijana kupotoka imechangiwa na mambo yafuatayo.

1.Udekezaji.

Wazazi wengine hawatekeleza majukumu yao kikamilifu ya kuwarekebisha wanao wakati wanapokosa nidhamu.Wazazi hawa wamewafanya wanao kutoa athari za matendo maovu kwa sababu hawawaadhibu wanapotenda kosa bali wanawapapasa tu.

2.Ukosefu wa mifano bora kutoka kwa jamii na wazazi.

Baadhi ya wazazi wamewapatia mifano mibaya kwa wanao kwa kuwa wanashiriki katika kufanya matendo maovu mathalani ukahaba, unywaji pombe, uhalifu n.k

3.Ukosefu wa ustahimilivu.

Vijana wengi wamejipata wakitumia mihadarati maadamu wamekumbana na matatizo katika maisha yao na hivyo wanaona suluhisho ni kutumia dawa za kulevya.

4.Matumizi mabaya ya teknolojia.

Mitandao ya kijamii huwa na mambo mengine yanapotosha kwa kuwa baadhi ya watu huzitumia kusambaza mambo maovu kama vile video za ngono,video za uhalifu, vitabu vya ufuska.

5.Kutotosheleza mahitaji.

Kutotosheleza mahitaji k.m mavazi, chakula,maji n.k imechangia baadhi ya vijana kujihusisha na makundi ya uhalifu pamoja na mambo mengine yanapotosha kimaadili.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s