Skip to content

Category: Lugha na Sarufi

Itikadi za Waswahili.

Waswahili wana itikadi nyingi sana. Itikadi ni taasisi iliyo hai katika tamaduni za jamii zote za wanadamu. Ushirikina ni sehemu ndogo ya itikadi za watu.Uislamu na Ukristo haufunzi wa kuhimiza itikadi za ushirikina.Lakini baadhi ya waumini hujikuta wamejaa tele ndani ya uwanja huu wa maisha. Itikadi za waswahili wa mwambao wa Kenya ni pamoja na imani ya kuwepo pepo majini, mashetani n.k nguvu na uwezo wa pepo hao katika kulinda mashamba,mali,miji, kusaidia kutibu maradhi. Pamoja nazo Waswahili wana mila kama vile miiko mbalimbali.Kwa mfano kula gizani ni kula na shetani,… Read more Itikadi za Waswahili.

Ndoa na harusi za Waswahili.

Uswahilini,ndoa na harusi ni taasisi ya kwanza kwa uzito wa maisha ya kila siku ya mtu. Ubikira ni ada kubwa sana kwa wasichana waswahili kabla ya kuolewa kwani ndoa ndicho kitovu cha maisha ya waswahili. Huwa ni desturi iliyoenea mwote uswahilini wa wazazi na mashangazi kuwa washauri wakuu wa ndoa za watoto wao. Kuna hatua kadhaa tangu mtu aposapo hadi kutoa mahari na kufunga ndoa.Chuo hicho ndicho huwashirikisha makungwi na masomo katika kuwaelekeza na kuwafundisha wari harusi kabla na baada ya harusi. Kwa waumini wa kweli wa Uislamu sheria za… Read more Ndoa na harusi za Waswahili.

Mazishi ya Waswahili.

Mazishi ni taasisi ya kuwarejesha waja walikotoka ama na kuwakumbusha walio hai juu ya marejeo hayo kwa Mola wao. Msiba wa kifiliwa huwa ni faradhi-kifaya (faradhi ya kutosheleza).Kufiliwa huwa ni kazi kwa wote na kazi kubwa kwa majirani na marafiki ni kuwafariji jamaa ya waliofiwa. Kazi zote kuanzia uchimbaji kaburi, kupatikana kwa tusi, uchukuaji wa jeneza,uzikaji wa maiti na swala zote za kumsalia maiti ni za jumuiya. Maiti huoshwa na watu wake wa karibu na hapo ndipo utajua jamaa wa karibu wa marehemu kwani huyo ndiye ataingia jofuni.Huzuni ya kifo,kwa… Read more Mazishi ya Waswahili.

Mazishi ya Waswahili.

Mazishi ni taasisi ya kuwarejesha waja walikotoka ama na kuwakumbusha walio hai juu ya marejeo hayo kwa Mola wao. Msiba wa kifiliwa huwa ni faradhi-kifaya (faradhi ya kutosheleza).Kufiliwa huwa ni kazi kwa wote na kazi kubwa kwa majirani na marafiki ni kuwafariji jamaa ya waliofiwa. Kazi zote kuanzia uchimbaji kaburi, kupatikana kwa tusi, uchukuaji wa jeneza,uzikaji wa maiti na swala zote za kumsalia maiti ni za jumuiya. Maiti huoshwa na watu wake wa karibu na hapo ndipo utajua jamaa wa karibu wa marehemu kwani huyo ndiye ataingia jofuni.Huzuni ya kifo,kwa… Read more Mazishi ya Waswahili.

Nahau na maana zake

1.Amekula chumvi nyingi=ameishi miaka. mingi 2,Ana mkono wa birika=mtu mchoyo 3.Ametutupa mkono=amefariki,amekufa 4.Ameaga dunia=amekufa,amefariki 5.Amevaa miwani=amelewa 6.Amepiga kite=amependeza 7.Amepata jiko=kaoa 8.Amefumgapinguzamaisha=ameolewa 9.Anawalanda wazazi wake= kawafanana wazazi wake kwa sura 10.Kawachukua wazazi wake=anafanana na wazazi wake kwa sura na tabia. 11.Kawabeba wazazi wake=anawajali na kuwatunza wazazi wake. 12.Chemshabongo=fikiri kwa makini na haraka. 13.Amekuwa toinyo=hanapua. 14.Amekuwa popo=amekuwa kigeugeu 15.Ahadi ni deni=timiza ahadi yako 16.Amewachukua wazee wake= anawatunza vizuri wazazi 17.Amekuwa mwalimu=yu msemaji sana 18.Amemwaga unga=amefukuzwa kazi 19..Anaulimuwaupanga=anamaneno makali 20.Ameongeza unga=mepandacheo 21.Agiziarisasi=pigarisasi 22.Kuchungulia kaburi=kunusurika kifo 23..Fyatamkia=nyamaza kimya 24.Fimbo zimemwota mgongoni=ana alama za mapigo… Read more Nahau na maana zake

Visawe na maana zake.

Visawe ni maneno yenye maana sawa. *Neno=Kisawe* 1. Ardhi=Dunia 2.Ari=Nia 3.Aibu=Soni 4.Azma=Makusudio 5.Binti=Msichana 6.Chakula=Mlo 7.Chanzo=Sababu 8.Cheti=Hati 9.Chuana=Shindana 10.Chubua=Chuna 11.Chubuko=Jeraha 12.Chumvi=Munyu 13.Duara=Mviringo 14.Dunia=Ulimwengu 15.Familia=Kaya 16.Fedha=Hela/Pesa 17.Fukara=Maskini 18.Gari Moshi=Treni 19.Ghasia=Fujo 20.Ghiliba=Hila 21.Godoro=Tandiko 22.Hitimaye=Mwishowe 23.Herufi=Hati 24.Hesabu=Hisabati 25.Hodari=Bingwa 26.Idhini=Ruhusa 27.Jogoo=Jimbi 28.Jokofu=Friji 29.Kandanda=Soka 30.Kenda=Tisa 31.Kichaa=Mwendawazimu 32.Kileo=Pombe 33.Kimada=Hawara 34.Kiranja=Kiongozi 35.Kivumbi=Fujo 36.Kopoa=Zaa 37.Kongoro=Gema 38.Labda=Huenda 39.Labeka!=Abee!/Naam! 40.Laghai=Danganya 41.Lisanj=Ulimi 42.Majira=Wakati 43.Manii=Shahawa 44.Masalia=Mabaki 45.Mashaka=Tabu 46.Mbio=Kasi 47.Mchoyo=Bahili 48.Mdomo=Kinywa 49.Mlolongo=Foleni 50.Motokaa=Gari 51.Msimu=Majira 52.Mtima=Moyo 53.Mtindi=Maziwa Mgando 54.Mtindo=Staili 55.Mtu=Binadamu 56.Muda=Wakati 57.Mvuli=Mvulana 58.Nahodha=Kapteni 59.Nakshi=Urembo 60.Ndoa=Chuo 61.Ndondi=Masumbwi 62.Ndovu=Tembo 63.Nguo=Mavazi 64.Nguzo=Kanuni 65.Nia=Lengo 66.Nuru=Mng’ao 67.Nyanya=Bibi 68.Nyati=Mbogo 69.Ongea=Sema/Zungumza 70.Pombe=Mtindi 71.Raba=Kifutio 72.Rabana=Mola 73.Rafiki=Sahibu/Swahibu 74.Rehani=Poni 75.Rubani=Kapteni 76.Rundika=Tufika 77.Rushwa=Hongo 78.Saka=Winda 79.Sala=Dua 80.Samani=Fanicha… Read more Visawe na maana zake.

Mbona nisirudi.

Natamani nikarudi, siku zile zamani Ila tu imenibidi, uwezo sina sinani Nami ningejitahidi, pale ninapotamani Ila sasa nifanyeje, jua litarudi nyuma? # Natamani zama zile, zisokuwa na potole Lipopiga ukelele, nihudumiwe wavyele Ya kesho nisiyaole, vya shubiri nisivile Ila sasa nifanyeje, jua litarudi nyuma? # Mambo ya kukosa kazi, katu nisiyaelewe Kodi ikawe upuzi, nisikie kwa wenyewe Sinao hata mchuzi, nyumba nje kafungiwe Ila sasa nifanyeje, jua litarudi nyuma? # Lakini ningejipanga, kuyafanya maamuzi Singekuwa tena bunga, nikashinde kwa upuzi Kuovu singejiunga, ningeenda na wajuzi Ila sasa nifanyeje, jua litarudi… Read more Mbona nisirudi.